
Waukweli full
Wednesday, November 17, 2010
Happy birthday Jahflex

Wednesday, April 14, 2010
NAKAAYA AJIUNGA NA CHADEMA!


“Nchi yetu ina rasilimali za kutosha kabisa, hasa kwa upande wa madini ya Tanzanite ambayo yatosha kuwawezesha wananchi wote kuwa katika kiwango bora na kinachostahili kimaisha, mbali na vivutio vingine vya kitalii vilivyopo, lakini cha kushangaza mpaka hivi sasa, wapo Watanzania ambao wanaishi katika hali duni kimaisha na chini ya dola moja kwa siku,” alisema.Alisema, amejiunga na chama hicho hivi sasa na si mwaka jana ama mwaka juzi, kutokana na kuona hivi sasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania, jamii itamhitaji zaidi katika kuwahamasisha juu ya kujitambua katika haki zao za msingi, hasa katika masuala ya kisiasa.Vyombo vya habari vilimhoji mwanadada huyo kwa nini katika hatua za kwanza kwa lengo lake la kuamua kuingia katika siasa, ameamua kujiunga na chama hicho badala ya kuingia Chama tawala (CCM), au Chama cha Jamii (CCJ), alijibu kwa mshangao kuwa hajaona kama ni vyama ambavyo vipo kwa ajili ya kusaidia watu, bali ni kwa maslahi yao binafsi.

waliupongeza uamuzi wa msanii huyo kwa uthubutu wake wa kujiunga katika masula ya siasa bila woga wa aina yoyote ile, huku wakimuahidi kumruhusu kugombea nafasi yoyote ile ya uongozi, pindi atakapotimiza masharti na taratibu zote ndani ya chama.Viongozi hao walimkabidhi kadi ya uanachama na kumtaka kuwa makini sana, hasa katika kuhamasisha vijana wenzake, huku akiwashawishi wasanii wengine kuingia katika siasa na kuongea yale yote yanayostahili kwa haki kwa manufaa ya nchi yao."Ukiwa kama kijana mdogo sana na msanii ambaye ni kioo cha jamii, tunataka tuone bidii yako ya kuweza kufichua na kukemea maovu yote, utakayoyaona ndani ya vuguvugu la kisiasa ndani ya nchi yetu, ili jamii nayo iwe na imani na wanasiasa wake," alisema mmoja wa viongozi hao wa CHADEMA.Aidha, waliwataka wasanii wote nchini ambao wana uchungu wa kweli katika nchi yao, kujiunga kwa wingi katika chama hicho, ili kuweza kufikia na kutimiza lengo la kuwakomboa wananchi walio wengi masikini na sauti za wanyonge kusikika, hasa katika suala zima la kutatua matatizo yao ikiwa ni pamoja na umaskini.
Sunday, March 28, 2010
UNAMKUMBUKA JOHN MAHUNDI???
Producer Mkali afanyae kazi zake Marekani John Mahundi kwa sasa yupo Bongo baada kufiwa na Mama yake mzazi aliyefariki wiki iliyopita baada ya kupelekwa India kwa matibabu.Kwa sasa John yupo nyumbani na familia yake na pia anatoa shukurani kwa ndugu jamaa na marafiki kwa ushiriki wao katika kipindi hiki kigumu. Mungu ailaze pema roho ya Mama yetu mpendwa na pia awape nguvu familia ya Mahundi.Pia kuna Mikono yake inakuja soon kwani kwa sasa yupo katika studio ya Seductive Records akipika Beats zilizokwenda shule.Pichani ni John Mahundi kushoto akiwa na C.E.O wa Emptysoulz Poduction Solomon Lamba wakiwa Seductive Records
Thursday, March 18, 2010
K.I.U IZ WOW
Tuesday, November 3, 2009
Monday, September 21, 2009
Jaflex is wow in K.I.U
Subscribe to:
Posts (Atom)